img

FAWE TANZANIA

Empower Young Girls & Women to Access quality Education

Blog Details

Image
Image

sera za urejeaji na mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kuwarejesha shuleni wanafunzi waliokatiza masomo.

Shirika la FAWETZ limekuwa miongoni mwa wadau waliohudhuria uzinduzi wa taarifa ya tathmini ya sera za urejeaji na mpango wa utekelezaji wa mwongozo wa kuwarejesha shuleni wanafunzi waliokatiza masomo katika ngazi ya elimu ya msingi na sekondari kwa sababu mbalimbali, tukio lililofanyika jana tarehe 12/11/2025 Dar es Salaam, Serena Hotel. Mgeni rasmi akiwa ni Dr.Hussein Mohamed Omar, Naibu Katibu Mkuu Elimu – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

 

Uzinduzi huu una umuhimu mkubwa katika kuimarisha utekelezaji wa sera inayolenga kuhakikisha watoto wote, hususan wasichana waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito, umasikini au changamoto za kijamii, wanapata nafasi ya pili yakuendelea na elimu yao.

 

Hatua hii ni msingi muhimu katika kujenga mfumo wa elimu jumuishi unaotoa fursa sawa kwa kila mtoto na kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma kutokanana hali au mazingira aliyopitia. Uzinduzi huu pia unatoa dira kwa serikali na wadau kupanga mikakati endelevu yakutokomeza vikwazo vinavyowanyima watoto haki ya elimu.

FAWETZ itashirikiana na serikali pamoja na wadau wengine katika Kutekeleza mpango huo ilikuhakikisha watoto wote hususan wasichana wanapata haki yao ya msingi ya elimu na kutimiza ndoto zao.

 
 

Leave A Comment