- Written by: admin
- June 5, 2026
maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.
FAWE Tanzania tume endelea na maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia iliyofanyika tarehe 5/12/2025 Ijumaa. Katika Shule ya Msingi Magiri, mkoani Tabora, tukisisitiza katika umuhimu wa kulinda usalama wa watoto, hususan katika zama hizi za matumizi makubwa ya teknolojia.
Kupitia kutoa elimu, mijadala na maigizo ya wanafunzi, Wazazi na Walimu wamepata ufahamu kuhusu:
- Namna ya kutambua na kupinga ukatili wa kijinsia.
- Usalama wa kimtandao kwa watoto, kuepuka uonevu, vitisho na maudhui hatarishi.
- Kujiamini na kuripoti vitendo vya ukatili kupitia mifumo salama ya taarifa.
- Kujenga utamaduni wa kuheshimiana na kutetea haki za wasichana na wavulana shuleni.
Kauli mbiu ya mwaka huu “Ungana Kutokomeza Ukatili wa Kidijitali Dhidi ya Watoto, Wasichana na Wanawake” imesisitizwa kwa nguvu ilikuhakikisha kila mtoto anatumia teknolojia kwa usalama na kwa manufaa. Tunaamini kwamba shule ni mahali salama pa kujifunza bila vitisho, ubaguzi wala ukatili.
Pamoja tunaweza kutokomeza ukatili wa aina yoyote!
